Kwa picha: Idara ya uangalizi wa haram tukufu yakamilisha kazi ya kusafisha haram pamoja na kutandika mazulia mapya

Maoni katika picha
Miongoni mwa mkakati wa idara ya uangalizi wa haram tukufu yenye jukumu la kuosha kubba takatifu kila baada ya muda fulani, watumishi wa idara hiyo wamekamilisha kazi ya kuosha haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutandika mazulia mapya.

Kuhusu utendaji wa kazi hii tumeongea na kiongozi wa idara hiyo Ustadh Zainul-Aabidina Adnani Alquraishi amesema kua: “Watumishi wa kitengo chetu wamemaliza kazi ya kuosha haram tukufu ya mwezi wa bani Hashim (a.s) sambamba na kuosha vioo, maraya na mapambo kwa kutumia vifaa maalum.

Akaongeza kua: “Baada ya kumaliza kuosha tumefukiza na kupuliza marashi maalum ndani ya haram tukufu, na wala sio eneo la kaburi peke yake bali hadi kwenye marumaru kumepuliziwa aina maalim ya marashi”.

Akasema: “Baada ya kumaliza kuosha tumetandika zaidi ya mazulia (88) mapya, yenye ubora wa hali ya juu na yenye ukubwa tofauti, yana nakshi za mimea zinazo endana na utukufu wa eneo hili”.

Akamaliza kwa kusema: “Kawaida huwa tupo makini sana katika kuchagua muda muwafaka wa kuosha na kutandika mazulia, kazi hizo hufanywa usiku wa manane baada ya mazuwaru watukufu kupungua”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: