Kuanza kwa semina ya wasichana Yanabiiáh Rahmah

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za Quráni zinazo fanywa na idara ya ufundishaji wa Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya kidini ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, idara tajwa imeratibu semina ya wanawake yenye anuani isemayo: (Yanabiiáh Rahmah) ndani ya Sardabu ya Imamu Kaadhim (a.s) katika Ataba tukufu, semina maalum kwa ajili ya wakina dada wenye umri wa miaka (14) na kuendelea, chini ya ratiba maalum inayo endana na umri wa washiriki, nayo ni miongoni mwa semina zake za kiangazi zinazo lenga kutumia vizuri likizo za kiangazi, na kuwafanya wapende Quráni na kuithamini katika nafsi zao, sambamba na kutengeneza kizazi cha wasichana kinacho jua Quráni na kinacho weza kuishi kwa kufuata mafundisho ya Quráni tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa semina bibi Fatuma Saidi Abdu Hashim: “Kuna ratiba kamili yenye masomo tofauti na mihadhara ya: (Quráni sahihi, hukumu za usomaji wa Quráni, kuhifadhi Quráni tukufu) pamoja na kufasiri baadhi ya aya za Quráni sambamba na masomo ya Fiqhi, Aqida na vipindi vya mapumziko na mashindano na kutembelea sehemu za Ataba tukufu”.

Akaongeza kua: “Semina hii inafanyika siku nne kwa wiki, inasimamiwa na wasomi wenye uzowefu mkubwa wa semina za aina hii, kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwa kushirikiana na watalam wa kituo cha utamaduni wa familia”.

Kumbuka kua idara ya Quráni tawi la wanawake inatoa kipao mbele zaidi katika kufundisha Quráni tukufu kwa wasichana wote hasa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuwahimiza kufuata mwenendo wa Quráni tukufu, wawe na uwelewa sahihi unao endana na riwaya za Ahlulbait (a.s) pamoja na kuifanyia kazi katika maisha ya kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: