Marjaa Dini mkuu atoa wito wa kuboresha mazingira ya elimu ya Iraq na kutatua changamoto ya tatizo la ufaulu katika masomo

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya (15 Dulqaada 1440h) sawa na (19 Julai 2019m), iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Abdulmahdi Karbalai, amezungumza sababu za kushuka kiwango cha ufaulu hapa Iraq, na akaonyesha kusikitishwa na matokeo ya darasa la tatu sekondari (upili) yaliyo tangazwa na wizara ya malezi (tarbiyya) ya Iraq.

Kuhusu kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi amesema kua: “Hakika jambo hili linaumiza na linahitaji utatuzi wa haraka, hatukatai kua kuna baadhi ya wanafunzi wamefaulu kwa alama za juu –Allah awazidishie- lakini tukiangalia matokeo ya jumla yaliyo tangazwa na wizara tutakuta ufaulu wa wanafunzi umeshuka kwa kiwango kikubwa”.

Akaongeza kua: “Kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi kuna matokeo mabaya kwa wanafunzi wenyewe na wazazi/walezi wao na kwa taasisi za serikali, kwa nini? Kwa sababu kunashusha matumaini na kujiamini kwa kizazi hiki”.

Akatoa wito kwa wenye mamlaka, waangalie tatizo la uchache wa majengo ya shule na wahakikishe wanatatua tatizo la zamu zatu za wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: