Kwa kualikwa Atabatu Abbasiyya tukufu: Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu amekwenda kumtembelea na kumpongeza kwa kupewa madaraka hayo

Maoni katika picha
Ameitikia mwaliko tukoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Radhawiyya Mheshimiwa Shekh Ahmadi Marwi, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea Atabatu Radhawiyya akiwa na ujumbe mzito.

Sayyid Ahmadi Swafi amesifu mwaliko huo na kusema kua ni msingi mzuri wa kuongeza ushirikiano katika kuwahudumia mazuwaru wa malalo hizi tukufu, pia amemshukuru na kumpongeza Shekh Marwi pamoja na watumishi wa Atabatu Radhawiyya kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu wa nane (a.s).

Akatoa pongezi maalum kwa Shekh Marwi kwa kupewa madaraka ya kua kiongozi mkuu kisheria wa Atabatu Radhawiyya, akamtakia mafanikio mema na akamuomba Mwenyezi Mungu awape malipo mema kwa juhudi wanazo fanya.

Ziara hii ilikua na majadiliano mazuri baina ya Ataba mbili takatifu, Sayyid Swafi ameeleza mambo yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika kuhudumia mazuwaru na kuhakikisha wanafanya ibada zao kwa amani na utulivu, akafafanua kua lengo kuu la Ataba tukufu ni kutoa huduma bora kwa mazuwaru, hususan katika wakati za ziara ya Arubainiyya.

Kumbuka kua ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu umehusisha wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya, Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, rais wa kitengo cha mgahawa (mudhifu) Mhandisi Aadil Hamaami, rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nusir Muhammad Shahidi Dahani na mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika jamhuri ya kiislamu ya Iran bwana Muhammad Zaryuun.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: