Hatua ya mwisho… mradi wa kupanua Maqamu ya Imamu Mahadi (a.f) siku baada ya siku unaelekea kukamilika

Maoni katika picha
Kazi ya upanuzi wa Maqamu ya Imamu Mahadi (a.f) imepiga hatua kubwa, inaelekea kukamilika siku baada ya siku, muonekano wa mwisho umeanza kudhihiri, baada ya kukamilika vitu vingi katika ujenzi huo, yakiwa ni matunda ya juhudi kubwa zinazo fanywa na wahandisi chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, sehemu zote za nje na ndani zimekamilika kwa kiwango kikubwa.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi ya upanuzi wa Maqaamu ya Imamu Mahadi imeanza kukamilika kidogo kidogo, uzuri wake umeanza kudhihiri, sehemu mbalimbali za kazi hii zimefika katika hatua nzuri, kama vile:

  • - Uwekaji wa maraya katika paa (dari) na kwenye kuta.
  • - Uwekaji wa marumaru upande wa mbele na nyuma pamoja na kashi Karbalai.
  • - Kukamilika uwekaji wa mfumo wa umeme, utowaji wa tahadhari, zima moto, mawasiliano na ulinzi.
  • - Kazi zinaendelea kwenye milango mikuu, ukiwemo mlango mkubwa ulio katikati ya longo kuu la zamani kwa nje, wenye upana wa zaidi ya mita nne na pembezoni mwake kuna nguzo zitakazo wekwa kashi Karbalai, katika ujenzi huu yametumika maumbo ya chuma ambayo ni sehemu ya upanuzi mpya wa mradi huu.
  • - Kukamilika kwa ujenzi na uwekaji wa marumaru katika mnara wa saa uliopo sehemu ya mbele ya Maqaamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: