Idara ya maraya na mapambo chini ya kitengo cha uangalizi wa haram tukufu inafanya kazi ya kusafisha maraya na mapambo yaliyopo ndani ya haram tukufu, kwa namna ambayo wanahakikisha zinakua safi kila siku.
Kazi ya usafi inahusisha kutoa vumbi kwenye maraya na mapambo kwa kutumia vifaa maalum vya kusafishia vioo, sambamba na kutumia baadhi ya mitambo na winchi kwa ajili ya kufikia sehemu za juu ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kazi hii inasaidia kudumisha uzuri wa maraya na mapambo yanayo pendezesha malalo takatifu, na kuingiza furaha katika nafsi ya zaairu wakati wa kutekeleza ibada ya ziara.