Baada ya kupata mafanikio na kuona matunda yake: Ratiba ya kongamano la pili imeanza

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zinazo fanywa na kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa wanafunzi wa sekondari ni kuendesha makongamano ya mambo ya kitamaduni, baada ya kufanikiwa kwa kongamano la kwanza kamati imeamua kupanua wigo na kuandaa kongamano la pili kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala chini ya kauli mbiu isemayo: (Familia yangu ni amana yangu).

Mkuu wa kituo na rais wa kamati ya maandalizi Ustadhat Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tangu kuanzishwa kwa kituo cha utamaduni wa familia kuna mambo mengi tumekua tukiyapa kipaombele, likiwemo jambo la: kujali watu wa rika zote na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazo wakabili pamoja na kuikabili jamii kwa ujumla, na kutumia kipindi cha likizo za kiangazi kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwafundisha kujiamini na kujitegemea”.

Akaongeza kua: “Kongamano limekua na ratiba tofauti, kuna ratiba ya utowaji wa mihadhara elekezi pamoja na mihadhara ya kuelezea historia ya Atabatu Abbasiyya tukufu na miradi yake, sambamba na mijadala mbalimbali baina ya wanafunzi inayo lenga kuwajenga katika masomo ya Fiqhi, Aqida, Sira na lugha ya kiarabu”.

Akabainisha kua: “Tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi na wameonyesha kufurahishwa na ratiba ya kongamano hili, ukizingatia kua linasimamiwa na kuendeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu yenye uzowefu mkubwa katika mambo haya”.

Kumbuka kua kongamano hili ni miongoni mwa program za kitamaduni zinazo simamiwa na kuendeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lengo la kutengeneza kizazi chenye maadili mema, walengwa wakuu ni wanafunzi wa shule za sekondari katika mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: