Maahadi ya taaluma na kukuza vipaji Alkafeel yaendesha warsha kwa watumishi wa chuo cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Maahadi ya taaluma na kukuza vipaji Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya inaendesha warsha kuhusu program ya uhasibu waliyo tengeneza.

Warsha hii ni kwa ajili ya watumishi wa kitengo cha mali na wahasibu wa chuo cha Al-Ameed, hii ni kutokana na namna viongozi wa chuo wanavyo tilia umuhimu kuongeza uwezo wa watumishi wao na kutatua changamoto za kiutendaji katika idara za chuo.

Mkuu wa Maahadi ya Alkafeel Ustadh Saamir Swafi amesema kua: “Kutokana na maombi tuliyo pata kutoka chuo cha Al-Ameed kuhusu kutoa mafunzo ya uhasibu na utunzaji wa mali, tumeandaa warsha kwa ajili ya watumishi wa vitengo hivyo, wameelezewa mambo yote ya utangulizi kuhisi uhasibu na namna ya kuandaa vielelezo vya malipo”.

Akaongeza kua: “Katika warsha hii pia tumefundisha namna ya kupanga bei na thamani ya hela pamoja na namna ya kufanya kazi kwa ubia na mambo mengine”.

Fahamu kua Maahadi imepiga hatua kubwa katika kuandaa na kutengeneza App, na inawataalam wakubwa wa fani hiyo, tayali imesha tengeneza program nyingi za mambo mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: