Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amehimiza kuanzishwa kituo cha utafiti kitakacho kua na vifaa vya kisasa, kitakacho kidhi mahitaji ya walimu na wanafunzi pamoja na kuendeleza utafiti hapa nchini.
Amesema hayo alipo tembelea chuo cha Al-Ameed na kukutana na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Hassan Jaabir pamoja na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na akakagua mafanikio yaliyo fikiwa na chuo.
Katika kikao hicho wamejadili mafanikio ya kielimu yaliyo patikana pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla katika mwaka huu kwa wanafunzi, sambamba na kuangalia kiwango cha mafanikio ya miradi inayo fanywa na chuo kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya, ukiwemo ujenzi wa bweni za wanafunzi wa kike pamoja na kumbi za darasa na maabara ambazo zinakaribia kukamilika.
Amepongeza kazi zinazo fanywa na kamati ya maandalizi ya kuandaa kongamano la kwanza kuhusu huduma za kidaktari katika ziara ya arubainiyya, litakalo simamiwa na chuo katikati ya mwezi wa Septemba ujao.
Kikao hicho kimehudhuriwa na makamo kiongozi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Mushtaqu Ali na Dokta Alaa Mussawi na mkuu wa kitengo cha rasilimali watu Ustadh Majidi Muhammad Rabii.