Mihadhara madhubuti imetolewa na jumuwiya ya Skaut ya Alkafeel katika program ya kujenga uwezo awamu ya tatu

Maoni katika picha
Jumuwiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa mihadhara mingi ya kimalezi na kiutamaduni kwa wanafunzi wanaoshiriki kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo awamu ya tatu.

Mihadhara hiyo ipo ndani ya ratiba ya mafunzo, mhadhara wa kwanza amezungumzia mada ya Aqida isemayo (Nafasi ya akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu), ulitolewa na kiongozi wa mikakati na mafunzo katika jumuwiya Dokta Zamani Kinani ndani ya ukumbi wa jengo la Sayyid Shuhadaa, ambalo lipo chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu, mada hiyo inamisingi ya falsafa katika kuelezea akili na kutumia dalili za kiakili katika kumtambua Mwenyezi Mungu pamoja na kufafanua ulazima wa Dini kwa binadamu, sambamba na kutaja tofauti kati ya Dini ya Mwenyezi Mungu na zisizokua zake.

Muhadhara wa pili ulikua unahusu kulipenda taifa, ulitolewa na Ustadh Jasaam Saidi, alizungumzia hatari kubwa inayo kabili taifa lisilokua na watu wazalendo, zikiwepo hatari za kidini, kimaadili na kiuchumi, pamoja na kutaja mifano ya hatari hizo katika maisha ya kila siku na uhusiano wake na uzalendo.

Muhadhara wa tatu ulikua unasema (Mafahimu za ibada) ulitolewa na Shekh Hassan Llami, ameongelea mafuhumu ya ibada na akafafanua kua ni jambo lililopo ndani ya akili ya kila mtu, kwani kila akili anajua jambo baya na zuri.

Mwisho ulikua muhadhara usemao (Athari ya ujinga katika maisha yetu ya kila siku) ulitolewa na Shekh Bahaau Ismaili, amezungumzia siri za misaada ya Mwenyezi Mungu katika maisha yetu, na athari yake katika elimu zingine zinazo kubalika katika maisha ya duniani”.

Mihadhara hiyo imepata mwitikio mkubwa kutoka kwa washiriki na wameuliza maswali mengi, ambapo wahadhiri walijibu maswali yote na kutoa ufafanuzi zaidi pale walipo takiwa kufanya hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: