Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimeanza kufunga feni za kunyunyiza maji kwenye barabara zinazo elekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kazi ya kufunga feni za kunyunyiza maji katika barabara zinazo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na maeneo yanayo zunguka haram tukufu.

Mradi huu umepewa jina la (Mradi wa feni za Hauraa) kutokana na kuongezeka kiwango cha joto katika msimu wa kiangazi, jambo ambalo limesababisha kitengo cha usimamizi wa kihandisi kutafuta njia ya kupunguza joto kwa mazuwaru watukufu.

Tumeongea na rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Mhandisi Samiri Abbasi ambaye amesema kua: “Mafundi wanaofanya kazi katika kitengo chetu wameanza kufunga feni katika maeneo yanayo zunguka haram tukufu na kwenye barabara zinazo elekea katika haram, wamesha funga karibu feni (350) zenye mabomba ya maji na umara mkubwa.

Akaongeza kua: “Tulianza kufanya kazi hiyo katika barabara ya Furat, tumefunga feni kwenye nguzo za umeme zilizopo barabarani, hali ya hewa imekua nzuri kwa asilimia (%70) ukilinganisha na hapo awali”.

Akasema: “Hali kadhalika katika maeneo yanayo zunguka haram tukufu, tumefunga karibu feni (50) za kunyunyiza maji, tutafunga pia feni zingine za kupuliza hewa ya baridi ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasema kua; mafundi wanaendelea na kazi ya kufunga feni hizo kwenye barabara zingine zinazo elekea katika malalo takatifu.

Akamaliza kwa kusema: “Wanafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kuhakikisha wanamaliza haraka kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu, utekelezaji wa mradi huu uko chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi, unafanywa na zaidi ya idara moja zilizo chini ya kitengo hicho”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: