Ugeni wa wanawake kutoka Lebanon: Maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu inapokea watu wa aina mbalimbali wanaokuja kuangalia vitabu, kusoma na kufanya utafiti

Maoni katika picha
Bibi Naahid Qabuut ambaye ni mjumbe wa kamati ya mahusiano ya Atabatu Husseiniyya nchini Lebanon ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu inapokea watu wa aina mbalimbali wanaokuja kuangalia vitabu, kusoma na kufanya utafiti, imekua msaada kwa wanafunzi wa fani zote, na inamchango mkubwa katika kuhifadhi turathi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuzidhihirisha katika namna bora inayo endana na utukufu wao.

Ameyasema hayo alipo fuatana na ugeni kutoka Lebanon uliokua na washindi wa shindano la mjukuu mkubwa, lililo fanywa na kituo cha Hauraa Zainab (a.s) chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu.

Akaongeza kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma za aina mbalimbali, hasa zinazo husu kumjenga mwanamke katika mambo tofauti, jambo hilo ni fahari kubwa, na idara ya wanawake ni ushahidi wa wazi wa jambo hilo”.

Naye bibi Asmaa Al-Abadi kiongozi wa idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika ziara hii ni moja kati ya ziara nyingi zinazo fanywa na watu tofauti kutoka ndani na nje ya Iraq, ugeni huu umetembelea sehemu za maktaba na wameangalia vitabu vilivyopo na machapisho mbalimbali, pamoja na kusikiliza maelezo kuhusu harakati zinazo fanywa na idara ya wanawake kuhusu wanawake, na juhudi kubwa za kuwajenga wanawake kielimu na kimaadili”.

Akaongeza kua: “Mwishoni mwa ziara ya ugeni huo, uliotembelea pia kituo cha kurepea nakala kale na makumbusho ya Alkafeel, na jengo la kibiashara la Al-Afaaf, walimeonyesha kufurahishwa na wamesifu walicho kiona”
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: