Wasomi wa kisekula na waandishi wa habari waitembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka mkoa wa Dhiqaar unao husisha wasomi wa kisekula na waandishi wa habari umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, kuangalia mafanikio yake katika sekta ya elimu, utamaduni na viwanda, wamefanya matembezi ndani ya korido za Ataba tukufu pamoja na makumbusho ya Alkafeel bila kusahau maktaba na Daru Makhtutwaat ya Ataba tukufu.

Rais wa ugeni huo Dokta Muslim Khuzáli amesema kua: “Tumekuja kutoka mkoa wa Dhilqaar kuitikia wito mtukufu wa Atabatu Abbasiyya, msafara wetu umehusisha wasomi wa kisekula na waandishi wa habari kwa lengo la kuimarisha mawasiliano, na kuangalia maendeleo ya Atabatu Abbasiyya katika nyanja tofauti.

Akabainisha kua: “Ziara yetu inafaida kubwa, baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za Ataba hususan maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya iliyo jaa hazina ya elimu za aina zote, sehemu nyingine muhimu kwetu ilikua ni katika makumbusho ya Alkafeel iliyo jaa vifaa kale vya thamani na adim ambavyo ni ushahidi wa yaliyo fanyika miongo na miongo”.

Akamaliza mazungumzo yake kwa kushukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni, kilicho chukua jukumu la kualika ugeni huu kwa ajili ya kuja kuangalia maendeleo ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua ziara hii ni miongoni mwa ratiba ya kupokea wageni mbalimbali wanaofanya kazi na Ataba tukufu, hupokewa wageni wa aina hii kutoka ndani na nje ya Iraq katika kipindi cha mwaka mzima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: