Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kufundisha mambo mbalimbali, katika ratiba ya kujenga uwezo awamu ya tatu, masomo ya hivi sasa yanalenga makumi ya wanaskaut na yamefundishwa kupitia mihadhara tofauti.
Mhadhara wa kwanza ulikua wa kidini wa somo la (Fiqhi, mada ya twahara na swala), ulitolewa na Shekh Ahmadi Shawili, amezungumza namna ya kujitwaharisha twahara kubwa na ndogo kwa kutumia maji au udongo, na akafafanua umuhimu wa swala katika maisha ya mwanadamu na akaelezea nguzo za shwala.
Mhadhara wa pili ulikua unahusu misingi miwili ya Dini, ambayo ni (Tauhidi na Uadilifu), ulitolewa na Shekh Muhandi Sahalani, akafafanua tauhidi katika dhati na tauhidi katika sifa, pamoja na kueleza uadilifu wa Mwenyezi Mungu, akatoa ushahidi mbalimbali na mifano ya kiakili pamoja na visa vinavyo endana na hisia.
Muhadhara wa tatu ulikua unahusu mambo ya kimaadili (Akhlaqi) ulikua una anuani isemayo: (Ukweli na uaminifu), ulitolewa na Shekh Hassan Laami, akafafanua umuhimu wa msema kweli na kutunza amana, akasema kua hayo ndio msingi wa maadili mema.
Muhadhara wa nne ukatolewa na Shekh Ahmadi Shawili, akaeleza (fiqhi ya michezo), akafafanua aina ya michezo inayo faa ikiwemo ya kielektronik. Pazia la mihadhara likafungwa kwa mhadhara wa (ukweli).
Halafu wakahitimisha ratiba ya Skaut kwa michezo mbalimbali ya kiakili.