Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wanaendelea na ujenzi wa jengo la vyoo katika barabara ya Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Bado mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na ujenzi wa jengo la vyoo katika barabara ya Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (300) jengo linalo jengwa lina ghorofa nne, hadi sasa wamemaliza hatua ya pili na limekamilika kwa asilimia %50.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Mhandisi Samiri Abbasi Ali amesema kua: “Mafundi wamemaliza hatua ya pili ya mradi wa jengo jipya la vyoo kwenye barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika hatua hiyo wamejenga umbo la jengo kwa vyuma (Steel structures) kwa muda wa siku kumu na wanafanya kazi zaidi ya saa (12) kwa siku”.

Akaongeza kua: “Jengo ni la ghorofa nne, linajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (300), ghorofa tatu ndio zitakazo kua na milango ya vyoo, jumla ya milango yote itakua (300), tunatarajia kukamilisha ujenzi huu kabla ya mwezi wa Muharam ili viweze kutumiwa na mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kuanzia mwezi wa Muharam”.

Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo muhimu, kina idara nyingi na kina mafundi na wahandisi wengi, kinafanya kazi muda wote, pamoja na kazi ya matengenezo kimesha fanya miradi mingi ya ujenzi mikubwa na midogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: