Miongoni mwa ratiba ya hema la (Ruhamaau bainahum): kitengo cha malezi na elimu ya juu kinaendesha mashindano ya kimaadili kwa watoto wa kituo

Maoni katika picha
Idara ya maelekezo ya kimalezi chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha mashindano ya kimaadili kwa watoto wa kituo cha (Ruhamaau bainahum) kinacho lea watoto waliokosa malezi ya familia, mashindano hayo yameandaliwa na walimu waliobobea katika elimu ya nafsi.

Mashindano haya ni sehemu ya ratiba iliyo andaliwa kwa ajili ya kuwapa watoto elimu na malezi bora yatakayo wasaidia katika Dini na Dunia yao, kulikua na maswali ya kidini yanayo chochea ushindani kati yao, maswali yalikua yanahusu Imamu Msubiriwa (a.f) na mambo yanayo takiwa wakati wa kumsubiri.

Ustadh Ahmad Hamidi ambaye ni miongoni mwa waratibu wa mashindano haya amesema kua: “Maswali ya mashindano haya yanatokana na masomo waliyo fundishwa kituoni (Ruhamaau bainahum) katika ratiba ya hema, maswali yote yanahusu Imamu Mahadi (a.f) na yanalenga kuwaepusha na mitazamo mibaya, yakahitimishwa kwa kutaja mambo yanano takiwa wakati wa kumsubiri Imamu Hujjat (a.f)”.

Kumbuka kua kituo cha (Ruhamaau bainahum) kinahusika na kulea waliokosa malezi ya familia, ni moja na kituo cha khairiyya (kusaidia) kinacho dhaminiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kipo sawa na vituo vingine vya khairiyya (kusaidia) vilivyo chini ya Ataba tukufu katika kusaidia jamii mbalimbali za wairaq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: