Kutokana na mwitikio wa mafunzo ya Skaut katika msimu wa likizo za kiangazi yaliyo pewa jina la (Mabinti wa Aqida), yanayo simamiwa na idara ya shule za wasichana Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kupokea idadi kubwa na kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi, tumewagawa washiriki kulingana na maeneo wanako toka, baada ya kumaliza awamu ya kwanza iliyo husisha wanavyuo kutoka (Barsa, Muthanna, Naswiriyya na Misaan), leo wamezindua awamu ya pili iliyo pewa jina la (Wabeba bendera) ambayo inahusisha wanavyuo kutoka (Najafu, Baabil na Karbala).
Tumeongea na kiongozi wa idara ya shule za Alkafeel Ustadhat Bushra Alkinani kuhusu mafunzo haya, amesema kua: “Lengo la mafunzo ni kujenga mawasiliano ya kielimu na kitamaduni baina ya wanafunzi, na kuhakikisha kipindi cha likizo wanakitumia kwa faida, ratiba ya masomo haya ni mwendelezo wa masomo yaliyo tangulia na kukamilisha mafanikio yaliyo fikiwa, kutokana na mwitikio kuwa mkubwa imelazimika tuwagawe wanafunzi katika hema tofauti, ili wanafunzi wengi zaidi waweze kushiriki”.
Akafafanua kua: “Kila hema linakua na ratiba yenye vipengele vingi, wanafundishwa mambo ya kifamilia, kiroho na kutembelea Ataba tukufu, sambamba na kufundishwa utowaji wa huduma ya kwanza, kazi za mikono na michezo, pia kuna usomaji wa Quráni na darasa mjadala linakua na maswali na majibu”.
Kumbuka kua ratiba hii ni moja ya harakati zinazo fanywa na idara ya shule za wasichana Alkafeel iliyopo katika kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), ambayo ni ratiba endelevu katika kipindi cha mwaka mzima, wanafunzi hufundishwa mambo mbalimbali, kwa ajili ya kuongeza uwezo wao kielimu na kijamii, hupambwa na mihadhara tofauti inayo wahimiza kufanya kazi na kutatua changamoto zinazo ibuka katika jamii.