Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kuwajali vijana kwani wao ndio nguvu kazi inayo tegemewa katika kujenga taifa, ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa amesema kua: “Tabaka la vijana linahitaji usimamizi maalum na kupewa kipaombele zaidi, nani awajibike, jambo hili ni tofauti, lakini jukumu ni la wote, kuna majukumu ya serikali, ambapo taasisi za serikali zinatakiwa zitekeleze majukumu yao, kwa kuwawekea vijana mazingira mazuri, kwa sababu vijana ni nguvu kazi muhimu inayo tegemewa katika ujenzi wa taifa, kuna baadhi ya kazi zinatakiwa zifanywe na vijana, pia taasisi za kiraia zinatakiwa kuwajibika, hali kadhalika familia lazima ziwajali vijana wao, ziwatengenezee mazingira mazuri na kuwaongoza, bila kusahau jamii, sisi kama jamii lazima tuonyeshe kuwajali vijana na kuwatengenezea mazingira mazuri”.