Katika nusu ya kwanza ndani ya mwaka huu: Zaidi ya ndoa (2400) zimefungwa na Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kua jumla ya ndoa kilizo fungisha ndani na nje ya mkoa wa Karbala zimefika (2458) katika nusu ya kwanza ya mwaka huu (2019).

Watu wamejitokeza kwa wingi kufunga ndoa kutokana na utakatifu wa eneo hili tukufu, hupenda kufanyia hapa sherehe pamoja na misiba yao pia, imekua kawaida ya familia nyingi za wairaq wanapo taka kufunga ndoa huja katika malalo hii tukufu wakitaraji kupata baraka za mwenye malalo hii katika ndoa yao.

Idara inayo husika na ndoa chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu imesema kua: “Namna ya ufungishaji wa ndoa katika haram tukufu huanza kwa kuwatambulisha wanandoa na familia zao, halafu husomwa khutuba ya ndoa kwa sauti inayo sikika tena kwa lugha fasaha ya kiarabu, ambayo husomwa na Sayyid au Shekh kutoka kitengo cha ndoa, kisha maharusi hupewa hati ya ndoa na nakala nyingine hutunzwa na idara, ndoa inayo fungwa ndani ya Atabatu Abbasiyya inatambulika na kukubalika na serikali ya Iraq chini ya sharia za raia wa Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: