Baada ya siku zilizo jaa harakati mbalimbali: Kongamano la maarifa lakamilisha ratiba yake

Maoni katika picha
Baada ya siku zilizo jaa harakati mbalimbali, kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na kamati ya maendeleo ya mwanamke katika mji wa Karbala imekamilisha ratiba ya kongamano la maarifa la pili kwa wasichana wanaosoma sekondari.

Hafla ya ufungaji wa kongamano likua na vipengele vingi, mada zilizo tolewa zilijikita katika malezi na utamaduni, zimelenga kujenga utamaduni wa wanafunzi, mada nyingi zimezungumzwa, mada ya Fiqhi imetolewa na bibi Fatuma Abbasi kutoka idara ya maelekezo ya kidini upande wa wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ameelezea namna ya kujiepusha na matatizo ya nafsi na jamii na umuhimu wa kutambua baadhi ya hukumu za kisheria zinazo endana na umri wao, kwa ajili ya kujilinda na baadhi ya fikra potofu.

Na kupambana na fikra mbaya zinazo sambazwa na mitandao ya mawasiliano ya kijamii na michezo ya kielektronik, kulikua na mada isemayo (Teknolojia za kisasa na athari yake katika afya) iliyo wasilishwa na Dokta Iqbaali Abul-Hubbi, akafafanua kua asilimia kubwa ya maradhi ya mwili na akili yanatokana na ongezeko la umeme katika ubongo linalo sababishwa na matumizi ya vifaa vya kielektronik, na kupelekea mtu kushindwa kuwa na maamuzi juu ya vitendo vyake.

Mwalimu wa maadili Adhraa Abbasi aliandaa mashindano ya kielimu ambapo kulikua na vikundi viwili ambavyo ni (Faidhu Zaharaa) na (Ummul Banina), kikundi cha (Faidhu Zaharaa) kikaibuka mshindi na wanakikundi wakapewa zawadi.

Hafla ikahitimishwa kwa kusikiliza risala iliyo andaliwa na wanafunzi walio shiriki, waliandika ujumbe wa Imamu Mahadi (a.s), kisha zikachaguliwa jumbe bora kumi na tano na waandishi wa jumbe hizo wakavishwa taji chini ya kauli mbiu isemayo: (Wasubiriaji wa kweli.. kutoka katika maidhar hadi kwenye jauhar), na ukatolewa waraka wa kutambua mchango wa washiriki wa kongamano, halafu wakapewa vyeti vya ushiriki.

Kamati inayo simamia kongamano hili imetangaza kua ipo katika maandalizi ya kongamano la tatu litakalo anza katikati ya mwezi ujao, na wametoa wito kwa anayetaka kushiriki awasiliane nao kwa simu namba (07828884555) namba hiyo pia inapatikana katika (Viber, Whatsapp na Telegram) au (07730124335/ 07730134335), pia unaweza kujiunga kwenye kikundi cha Telegram kiitwacho (Thaqafa ausaria) au kupitia linki ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: