Baada ya mafanikio yaliyo patikana chini ya mafundi mahiri wanaofanya kazi katika kiwanda cha Saqaa cha kutengeneza milango na madirisha ya makaburi na mazaru matukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, mafundi wamemaliza kazi waliyo pewa ya kuweka vipande vya dhahabu walivyo tengeneza sehemu ya juu ya dirisha la Maimamu wawili Aljawadaini (a.s).
Walianza kazi hiyo baada ya uongozi mkuu wa Atabatu Kadhimiyya kuamua kuweka dhahabu katika dirisha la Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) ili kulifanya liendane na utukufu wake, ndipo wakafanya makubaliano na Atabatu Abbasiyya tukufu na kukipa jukumu la kutengeneza vipande vya dhahabu na mina kiwanda cha Saqaa.
Makamo mkuu wa kiwanda cha Saqaa Ustadh Husaam Muhammad ameongea na mtandao wa kimataifa Alkafeel na kusema kua: “Tulianza kazi ya kutengeneza vipande vya dhahabu na mina kwa ajili ya kuweka sehemu ya juu ya dirisha takatifu, pamoja na vipande vya fedha vinavyo wekwa sehemu ambayo haifikiwi na mikono ya mazuwaru watukufu, sambamba na kufanyia matengenezo sehemu zilizo kua zimeanza kuharibika, mafundi wamefanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kuhakikisha wanamaliza kazi ndani ya muda uliopangwa katika mkataba”.
Fahamu kua mafundi wamefanikiwa kumaliza kazi yao ndani ya muda uliopangwa katika mkataba ambao ni siku (60), wametumia karibu kilo (12) za dhahabu na ayaar 24, kiwanda cha Saqaa kinauzowefu wa kutengeneza madirisha ya aina hii, kwani kimesha wahi kutengeneza dirisha la malalo ya Shekh Mufidi na Shekh Tusi.