Siku mpya ya (vituo vya kiangazi) katika bustani za chuo kikuu cha Al-Ameed kwa wanafunzi wa shule za msingi

Maoni katika picha
Ratiba ya masomo na shughuli za kimalezi inayo tekelezwa na shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea, inalenga kutumia vizuri kipindi cha likizo za wanafunzi za wavulana na wasichana, ratiba ya (vituo vya kiangazi) inatekelezwa kwa muda wa mwezi mzima siku tano kila wiki na imekua desturi ya kila msimu wa kiangazi.

Ustadh Manna Waaili mkuu wa shule ya msingi Al-Ameed amesema kua: “Kwa ajili ya kunufaika na wakati wa faragha kwenye kipindi cha likizo za shule za msingi tumeandaa ratiba inayo jumuisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na masomo ya Dini, michezo, mashindano, kuangalia sinema mbalimbali za mafundisho ya kimalezi, halafu wanafunzi hupelekwa kupumzika (kubarizi) katika mji wa Zaairina, na hulala katika majengo ya chuo kikuu cha Al-Ameed”.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa shule za wasichana Al-Ameed Ustadhat Minna Waaili zimeandaliwa nafasi maalum za mayatima katika ratiba hii.

Fahamu kua kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu huwapa umuhimu mkubwa watoto, kwa kuwawekea ratiba na mafundisho mbalimbali ya kimalezi, kidini na kimichezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: