Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa misaada kwa wapiganaji waliopo katika uwanja wa mapambano

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ofisi zake zimesambaa katika mikoa tofauti ya Iraq, inaendelea kutoa misaada kwa wapiganaji waliopo katika uwanja wa vita, ofisi ya mkoa wa Diyala imetoa misaada kwa wapiganaji wa kikosi za Abbasi (a.s) Liwaau/26 Hashdi Shaábi na wapiganaji wa serikali waliopo katika mkoa huo, katika mji wa Kanáan wanao pambana na mabaki ya magaidi, wamewapa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula, misaada hiyo inawasaidia kuendelea kupambana na magaidi.

Wakati huohuo ofisi ya ustawi wa jamii tawi la Bagdad nayo imetoa misaada kwa wapiganaji wa majini waliopo upande wa kusini wa mkoa huo, wamesaidia Liwaa Qamaru Ashira (a.s), kwa kuwapa kiasi kikubwa cha vyakula na matunda, kama sehemu ya kuenzi ushindi uliopatikana kutokana na damu za mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Shaábi.

Wapiganaji wameshukuru sana misaada endelevu na mikubwa wanayo pewa na idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: