Kutandikwa kwa ardhi

Maoni katika picha
Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!* Akainua kimo chake na akaitengeneza vizuri* Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake* Na juu ya hivyo ameitandika ardhi) maana ya neno la kiarabua (Dahw) ni kutandika na kunyoosha, na ikajaliwa kua mahala pa kuishi, Shekh Muhammad Jawaad Mughniyya anasema katika tafsiri Alkashaaf: aliitandika na kuinyoosha na kuifanya kua nzuri kwa kuishi na kutembea juu yake, na katika kitabu cha (Kujaribu kufahamu zama za Quráni) kinasema: neno (Dahaahaa) linamaana kua; ardhi imeumbwa kama yai, maana hiyo inakubaliana na vikra za wanajografia wa zama hizi.. neno (daha) pia linamaana ya kutandika, nalo ni neno pekee la kiarabu lenye maaya ya kutandika na umbo la yai kwa pamoja, hivyo linamaanisha kua ardhi imetandikwa na wakati huo huo inaumbo la duara kama yai, huu ni ufasaha wa hali ya juu wa kuchagua neno makini.

Kutoka kwa Imamu Ali Kiongozi wa waumini (a.s) anasema: (Hakika rehema ya kwanza iliyo telemka kutoka mbinguni hadi ardhini ilikua mwezi ishini na tano Dhulqaada, atakayefunga siku hiyo na akaswali usiku huo, ataandikiwa thawabu za kufanya ibada miaka mia moja, watu watakao kusanyika siku hiyo na kumtaja Mola wao mtukufu, hawataachana hadi kila mmoja apewe anacho kiomba, katika siku hiyo huteremswa rehema elfu elfu (laki moja), asilimia tisini na tisa ni kwa ajili ya waliomtaja Mwenyezi Mungu, walio funga na kuswali katika siku hiyo).

Sehemu ya kwanza kuumbwa katika ardhi ni sehemu ya Maka takatifu, kisha Mwenyezi Mungu mtukufu akatandika ardhi kwa kuanzia sehemu hiyo, na hiyo ndio maana ya kutandikwa ardhi kwa kuanzia katika Kaaba, jambo hili linathibitishwa na baadhi ya riwaya zilizo pokewa kutoka kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) imepokewa kua ardhi ilitandikwa miaka elfu mbili baada ya kuubwa kwake.

Katika kitabu cha Mafatihu Janani kilicho andikwa na Shekh Abbasi Qummiy imeandikwa kua, siku hii inaibada maalum za kufunga, kumtaja Mwenyezi Mungu, kuoga, pia kuna swala maalum: nayo ni rakaa mbili, unaiswali katika muda wa Dhuha, utasoma Alhamdu mara moja na suurat Shams mara tano katika kila rakaa, baada ya salamu useme: (Laa haula walaa quwata illaa billahil-aliyul-adhim) kisha uombe dua hii: (Yaa muqiila athraati aqilni athratii, yaa mijiiba da’waatii ajib daáwatii, yaa saamia aswaati ismaá swautii, warhamni wa tajaawaz sayyiaatii wamaa indii yaa dhaljalali wal-akraam).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: