Kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya awahutubia mubalighaat: Yatupasa kuufanya mradi wa uhadhiri na tablighi kuwa jambo la lazima kwa wanafunzi

Maoni katika picha
Shekh Abdu Swahibu Twaaiy mkuu wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kua: “Yapasa jambo la uhadhiri na tablighi kuwa la lazima kwa wanafunzi, jambo la msingi kwa kila mwanafunzi liwe ni kufundisha Aqida, Akhlaqi, Fiqhi na masomo mengine katika jamii”.

Ameyasema hayo alipo kutana na kundi la wahadhiri na mubalighaat katika sardabu ya Alqami ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, akasisitiza pia umuhimu wa kuwapa kipaombele zaidi wanawake katika malezi ya familia, akalinganisha kati ya wanawake wa zamani na wa sasa katika maendeleo haya ya kiteknolojia yaliyo jaa mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Akasema kua: “Lazima kuangalia majukumu ya mke katika familia, na kulinda siri za familia, kutofanya hivyo inaweza kua sababu ya kuvunja familia”.

Akabainisha kua: “Wanafunzi wa kike ni jukumu lingine, lazima uzingatiwe uwezo wao wa kufanya kazi za nyumbani na shuleni, haifai kuacha kufanya jambo la wajibu kwa ajili ya mustahabu”.

Makamo kiongozi Ustadhat Taghridi Abdul-Khaliq Tamimi amesema kua: Miongoni mwa vipaombele vya idara ya wahadhiri wa Husseiniyya ni kufanya makongamano na mikutano mbalimbali, kwa ajli ya kujadili na kuweka mikakati na ratiba, na kwa ajili ya kufaidika na elimu za wahadhiri wa Husseiniyya, Shekh Twaaiy anafuatilia kwa karibu maendeleo ya wahadhiri, kwani huwa kuna mihadhara ya aina mbalimbali inayo lenga kuendeleza tablighi katika sekta ya wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: