Watumishi wa Saaqi wahitimisha kugawa maji kwa mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu takatifu na wanaelekea Kadhimiyya tukufu

Maoni katika picha
Baada ya kutoa huduma mfululizo kwa muda wa siku zaidi ya kumi na tano, idara ya maji chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kukamilisha kazi ya kugawa maji kwa mahujaji watukufu, baada ya kuwapa maelfu ya lita ya maji ya baridi kutoka katika kituo cha (RO) pamoja na mamia ya vipande vya barafu kutoka kwenye kiwanda kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkuu wa idara hiyo bwana Ahmadi Hanuun ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kauli mbiu inayo tumiwa na watumishi wa idara ya maji inasema (Kuwapa maji mahujaji ni fahari kwetu), kazi hiyo ilianza tangu msafara wa kwanza kupita katika barabara ya (Nakhibu – Ar-Ur), watumishi wetu wamegawa maeflu ya maji safi ya kunywa kutoka katika kituo cha (RO) pamoja na mamia ya vipande vya barafu, kazi zote wameshirikiana na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) kilicho beba jukumu la kulinda barabara inayo tumiwa na mahujaji”.

Akaongeza kua: “Tuliweka mkakati maalum wa utekelezaji wa kazi hii ambayo ni utukufu mkubwa kwetu sambamba na kuwatumikia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kua kiongozi wetu Abulfadhil Abbasi (a.s) alikua mnyweshaji wa maji, na sisi tumechukua jukumu la kuwapa maji ya kunywa mahujaji watukufu wanaopita katika mji wa Karbala, tumegawa maji kwa misafara yote bila usumbufu, watumishi wetu walikua wanashindana katika kutoa huduma”.

Akasema kua: “Baada ya kumaliza kugawa maji kwa mahujaji sasa tutaelekea katika mji wa Kadhimiyya kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru wanao kwenda kufanya ziara huko katika kipindi cha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad (a.s), ikiwemo huduma ya kugawa maji ya baridi kwa kushirikiana na sekta husika katika mji huo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: