Zaidi ya wanafunzi (1800) wanahitimisha kozi za Quráni katika msimu wa kiangazi

Maoni katika picha
Tawi la Maahadi ya Quráni tukufu katika wilaya ya Khadhar mkoani Muthanna limefanya hafla ya kuhitimu kwa zaidi ya wanafunzi (1800) walioshiriki katika kozi za Quráni msimu huu wa kiangazi, ambapo wamesomeshwa Quráni tahfiidh na tilaawah pamoja na masomo ya Fiqhi, Aqida na Akhlaqi, masomo hayo yalidumu kipindi chote cha likizo chini ya selebasi maalum iliyo andaliwa na walimu bobezi katika Quráni.

Hafla ya kufunga semina iliyo fanyika katika Husseiniyya ya Imamu Almuntadhir (a.s) imepata mahudhurio makubwa ya wanafunzi na wazazi wao, sambamba na wakufunzi wao na ugeni ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya akiwemo Shekh Muhammad Ambaar muwakilishi wa Maahadi ya Quráni tukufu, ambaye aliongea kuhusu nafasi ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kusaidia vijana kwenye mambo ya kidini au kitamaduni, pia kulikua na nafasi ya usomaji wa Quráni ambayo ndio msingi wa kila kitu, bila kusahau ndio mhimili mkuu wa Dini na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), akaelezea pia umuhimu wa semina za Quráni za kiangazi ambazo hufanywa kila mwaka, na mwaka huu tumeshuhudia ushiriki wa wanafunzi (22,000) kutoka mikoa iliyo shiriki katika mradi huu, wakiwemo hawa ambao tumeshiriki katika hafla ya kuhitimu kwao na tunawaombea maendeleo mema.

Hafla ilipambwa na maigizo mawili, igizo la kwanza lilikua linasema: (Khofu na utashi) walionyesha fikra ya khofu ambayo hupatikana kwa vijana kinyume na matashi yao, ambapo wanatakiwa wasimamie matashi yao bila khofu ili waweze kupata mafanikio. Igozo la pili lilikua linasema: (Swala yangu ndio maisha yangu) lilionyesha namna ya kudumisha swala kwa wakati wake na kutompa nafasi shetani, wakahitimisha kwa shairi kutoka kwa Sajjaad Zarijaawi lililokua likihimiza kuwapenda Ahlulbait (a.s) na taifa letu kipenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: