Atabatu Abbasiyya tukufu yawekwa mapambo meusi katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuomboleza kifo cha Imamu Aljawaad (a.s) na mwendelezo wa harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu katika kukumbuka misiba ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) pamoja na dhulma walizo fanyiwa, Atabatu Abbasiyya imewekwa mapambo meusi katika korido na kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yanayo ashiria huzuni.

Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wapo katika huzuni. Mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaada mwaka (220h) ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa tisa Muhammad bun Ali Aljawaad (a.s), aliye uliwa na Mu’taswimu Abbasiy na msiba huo kuombolezwa na viumbe wa mbinguni kabla ya viumbe wa ardhini.

Kumbuka kua Imamu Aljawaad (a.s) alizaliwa katika mji wa Madina mwezi kumi Rajabu mwaka (195h), alichukua madaraka ya Uimamu akiwa bado mdogo, alikua na umri wa miaka (7) au (8), kipindi cha Uimamu wake kilidumu kwa miaka (17), majina yake ya laqabu ni: Aljawaad, Attaqiyyu, Alqaaniu, Azzakiyyu na Baabul-Muraad. Aliuwawa mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaada mwaka wa (220h) kwa sumu chini ya amri ya Mu’taswimu Abbasiy. Jafari bun Ma-Amuun alimshawishi dada yake Ummul-Fadhil aliye kua mke wa Imamu Aljawaad (a.s), naye Ummul-Fadhil alikua na ugonvi na mke mwingine wa Imamu ambaye ni mama wa Imamu Alhaadi (a.s), akakubali kumuua mume wake, akachukua sumu kali na akamuwekea kwenye chakula, Imamu (a.s) alipokula chakula hicho alihisi maumivu makali sana, Ummul-Fadhil akajuta na akalia sana kwa kitendo chake hicho, Imamu akamuambia: (Wallahi utapatwa na ufakiri wakudumu na balaa lisilo isha), akapata maradhi katika mwili wake, akamaliza mali zote kwa ajili ya kujitubu na wala hakupona, na Jafari bun Ma-Amuun alianguka ndani ya kisima kirefu akatolewa akiwa amekufa. Imamu (a.s) alikutana na baba zake watakatifu (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu (Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kweke tutarejea)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: