Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi amesema kua wanatekeleza wajibu wao wa kulinda amani na kutunza sifa yake pamoja na kulinda damu za mashahidi na haki za raia, akabainisha kua kikosi kinafanya kila kiwezalo kwa ajili ya kuweka vizuri mazingira ya Hashdi Shaaábi na kutunza sifa yao ya kujitolea.
Ameyasema hayo alipokua anapokea viongozi wa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) –Liwaau/26 Hashdi Shaábi- mbele ya wakuu wa idara wa Hashdi Shaábi katika makao makuu ya kikosi yaliyopo ndani ya jengo la Alqamiy katika mji mtukufu wa Karbala, Shekh Maitham Zaidi amekutana na wakuu hao na kujadili nao kuhusu hali ya sasa pamoja na kuimarisha ushirikiano baina yao, akawapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri wanayo fanya ambayo inatunza sifa ya Hashdi Shaábi na kulinda haki za raia.
Kituo cha habari cha kikosi cha Abbasi (a.s) kimesema kua, mkuu huyo amesema: “Kikao hicho kimejadili pia kuhusu mishahara ya wapiganaji, ambapo kikosi kilikua cha kwanza kutekeleza swala hilo”.
Akasisitiza kua: “Kikosi cha Abbasi (a.s) kitashiriki kila hatua ya maelekezo yanayo tolewa na uongozi mkuu wa jeshi na wakuu wa vitengo yanayo lenga kuboresha mazingira ya Hashdi kitaasisi”.