Jioni ya jana Jumanne (27 Dhulqaada 1440h) sawa na (30 Lulai 2019m) imefanyika shighuli ya kubadilisha bendera ya Maimamu wawili Aljawadaini (a.s), kama tangazo la kuanza msimu wa maombolezo ya kifo cha Imamu wa tisa Muhammad Aljawaad (a.s).
Shughuli hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Kadhimiyya na kuhudhuriwa na ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Haidari Shammariy akatoa tamko la ukaribisho, na akazungumza kuhusu tukio la kusikitisha katika nyoyo za waumini, kifo cha Imamu Muhammad bun Ali Aljawaad (a.s), na akazungumza kuhusu jukumu la vijana katika jamii, ukizingatia kua Imamu Aljawaad alichukua madaraka ya Uimamu akiwa na umri mdogo, na akauwawa kwa sumu akiwa bado kijana mdogo mwenye miaka (25).
Miongoni mwa aliyo sema katika khutuba yake ni: “Hakika majukumu yetu katika kipindi hiki cha Ghaiba yanaongezeka siku baada ya siku, kila mitihani inavyo ongezeka na vita ya kiitikadi na kitamaduni, ndivyo kinavyo ongezeka kiwango cha majukumu kwa kila mtu kutokana na nafasi yake katika jamii, taasisi za Dini zina nafasi kubwa ya kuelekeza na kurekebisha mambo yanayo potoshwa, ukizingatia tupo katika zama za kumsubiri Imamu Mahadi (s.f), na taasisi za malezi pia zinatakiwa kufanya jukumu hilo na kuwa msaada kwa vijana wa kiume na wa kike, bila kusahau nafasi ya vyombo vya habari katika kufundisha maadili mema, na kuhuisha utiifu kwa Imamu Mahadi (a.f) kila siku na kila muda”.
Baada yake ukafuata ujumbe kutoka kwa muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Kadhimiyya Dokta Ali Shukriy ambaye aliongea kwa niaba ya Shekh Hussein Aali-Yasin, katika maneno yake amezishukuru Ataba tukufu za Iraq sambamba na kukumbusha tukio la msiba linalo pelekea kubadilisha bendera.
Halafu likafuata shairi kutoka kwa Riyaadh Abdul-Ghina Alkadhimiy, kisha ikaimbwa kaswida ya kuomboleza na bwana Husseini Karraar Alkadhimiy, na kuhitimisha na muimbaji mashuhuri bwana Baasim Karbalaiy.