Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia mradi wa usomaji wa Quráni katika vyuo vikuu na Maahazi za Iraq, inaendesha mafunzo ya Murtadha (a.s) ambayo yanahusisha masomo mengi ya maarifa ya Quráni tukufu, Aqida, Fiqhi na mbinu za ufundishaji, kwa kushiriki zaidi ya wanafunzi (45) kutoka vyuo tofauti vya Iraq chini ya walimu waliobobea.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa kila kitu kinacho hitajika na wanafunzi kwa ajili ya kufanikisha masomo hayo, yanayo tarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tano ndani ya jengo la Maahadi ya Quráni tukufu, katika siku ya kwanza wamefundishwa mambo mengi kuhusu Quráni na namna ya kupambana na changamoto za ujana.
Wanafunzi wameshukuru sana Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Quráni kwa kuwapa masomo haya, yanayo wawezesha kuifahamu Quráni tukufu na kusambaza nuru yake katika jamii, wakasema kua walikua na haja kubwa ya masomo ya aina hii.
Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya inaendelea kufanya miradi inayo husu Quráni ndani ya mwaka mzima, kwa watu wenye umri tofauti na viwango mbalimbali vya elimu.