Imamu Muhammad Aljawaad ni mlango wa elimu na mlango wa Muraad

Maoni katika picha
Jawaad, Naqiyyu, Taqiyyu, Zakiyyu, Qaanii ni mlango wa haja kwa wafuasi na wapenzi wake, ni Imamu wa tisa baada ya Mtume (s.a.w.w), naye ni mlango wa Muraad, alikua muendelezaji wa mwenendo wa baba zake na babu zake, alisimama imara kuzuwia kila aina za uzushi na fikra potofu zilizo zuka katika zama zake pamoja na udogo wa umri wake.

Hakusalimika na chuki za bani Umayya na bani Abbasiy, watawala wa zama zake walimpiga vita kutokana na kuipenda kwao dunia, hadi akauwawa kwa sumu aliyo pewa na mke wake Ummul-Fadhil binti Ma-Amuun, Imamu (a.s) alifariki kwa sumu mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaada mwaka wa (220h) akiwa katika kilele cha umri wa ujana.

Alizikwa katika mji wa Bagdad jirani na babu yake Imamu Mussa Alkadhim (a.s), malalo zao hutembelewa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), na zimekua mlango wa haja kwa kila muumini.

Amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyo uwawa kwa sumu na siku atakayo fufuliwa kua hai na kutoa ushahidi juu ya walio mdhulumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: