Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetuma wapiganaji (60) kwenda kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) umekubaliana na kituo cha kufuta ujinga cha Karbala kuhusu kuwapeleka askari wake (60) walio soma katika madarasa ya kufuta ujinga kwenda kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi itakayo anza (4/ 8/ 2019), wakaashiria uwepo wa mradi wa kufuta ujinga na wanamkakati wa kujenga shule kwa jina la kikosi baada ya kuwasiliana na sekta zinazo husika.

Kiongozi wa kitengo cha maelekezo ya kidini na kufuta ujinga Shekh Qassim Juburiy amesema kua: “Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya kukutana na viongozi wa idara ya kufuta ujinga na malezi katika mkoa wa Karbala, hapo ukajadiliwa mradi wa kikosi cha Abbasi (a.s) unaolenga kufuta ujinga kwa baadhi ya wapiganaji wake, nao walionyesha utayali wao wa kushirikiana na kikosi katika kila jambo, ikiwemo kufungua shule kwa jina la kikosi cha Abbasi (a.s).

Fahamu kua ilifanyika warsha ya kujenga uwezo inayo husu kufuta ujinga chini ya anuani isemayo: (Kufuta ujinga ni jukumu la wote), na kusimamiwa na wizara inayo husika na kufuta ujinga kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s) na idara ya mkoa wa Karbala chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, yote hayo yamefanyika kutokana na juhudi za Atabatu Abbasiyya kupitia kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji za kuhakikisha elimu inaenea kwa jamii zote za wairaq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: