Kwa picha: Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanampa pole Imamu Hussein katika kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wake Aljawaad (a.s)

Maoni katika picha
Kwa huzuni na majonzi makubwa Adhuhuri ya Alkhamisi ya leo (28 Dhulqaada 1440h) sawa na (1 Agosti 2019m) Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Imamu wa tisa Muhammad bun Ali Aljawaad (a.s), matembezi hayo yameanzia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa malalo ya mwezi wa bani Hashim (a.s) walisimama kwa mistari huki wanaimba kaswida za kuomboleza zinazo elezea tukio hilo la kuhuzunisha.

Baada ya hapo wakaanza kutembea wakielekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakipiga vifua vyao na kutokwa na machozi kwa huzuni, walipo fika katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) wakafanya majlis ya kuomboleza pamoja na mazuwaru waliokua humo, huzuni ikatanda kama kawaida ya kila msiba katika watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu hufanya matembezi ya kuomboleza katika kila tukio la msiba wa mmoja wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: