Mawakibu za kuomboleza katika mkoa wa Karbala zinakumbuka kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s)…

Maoni katika picha
Kama kawaida yao katika kuomboleza vifo vya Maimamu watakasifu (a.s), asubuhi ya Ijumaa (29 Dhulqaada 1440h) sawa na (2 Agosti 2019m) Mawakibu za kuomboleza za Karbala zimehuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa tisa Muhammad Aljawaad (a.s).

Mawakibu zilianza matembezi ya kuomboleza mapema leo asubuhi kutoka sehemu mbalimbali za mji wa Karbala, na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu hiyo na kumpa pole Imamu wa zama (a.f).

Huku wakiwa na huzuni kubwa wameingia katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kumpa pole, kisha wakaelekea katika malalo ya baba wa watu huru (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu wakiwa wanaimba kaswida za kuomboleza na kupiga vifua vyoa na kububujikwa machozi, hadi walipo fika katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) wakafanya majlis ya kuomboleza.

Fahamu kua watu wa Karbala wamezowea kuomboleza misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa kufanya matembezi ya kuomboleza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: