Swala Ilaahu katika ndoa ya Twaahir… mwezi mosi Dhulhijja ilifungwa ndoa ya nuru mbili Ali na Fatuma (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya kwanza katika mwezi wa Dhulhijja mwaka wa (2) hijiriyya, ambayo ni sawa na siku ya leo, ilifungwa ndoa tukufu ya Imamu Ali na Fatuma Zaharaa (a.s) na kuitwa ndoa ya nuru mbili, tukio hilo linaumuhimu mkubwa kwa sababu wao ni watu muhimu na watukufu mno baada ya Mtume (s.a.w.w) matunda ya ndoa hiyo tukufu ni kupatikana kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), ndoa hiyo pia inaonyesha wazi nafasi ya Imamu Ali (a.s) mbele ya Mtume (s.a.w.w) kwani alimridhia kumuozesha mwanae tofauti na waumini wengine.

Imeandikwa katika hadithi iliyopo kwenye kitabu cha Kashfu Gumma kua, maswahaba wengi walijitokeza kutaka kumuoa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) lakini Mtume (s.a.w.w) aliwakatalia, alipokwenda kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) uso wake ulitabasamu na akafurahi sana, akasema: Hakuna mtu anayefaa kwa Fatuma ispokua Ali.

Akamuozesha kwa mahari ndogo, na shughuli ya haruli ya kawaida, aliwaozesha nuru kwa nuru, Fatuma akapewa vitu vichache vya kwenda navyo kwa Ali bun Abu Twalib (a.s), katika nyumba ambayo ndio kituo ambacho Mwenyezi Mungu alikiteuwa kuangazia dunia kwa nuru ya uislamu na Qur’ani, baada ya Mtume (s.a.w.w) kukamilisha mafundisho ya Dini, na kukamilisha neema kwa waislamu na Mwenyezi Mungu kuuridhia uislamu kua Dini ya walimwengu.

Kutoka kwa Khabaab bun Arti anasema: Hakika Mwenyezi Mungu alimwambia Jibrilu: Ndoa ya nuru kwa nuru, walii wake ni Mwenyezi Mungu, na mposaji ni Jibrilu, na mtangazaji ni Mikaeli, na mualikaji ni Israfiil, na msambazaji wa taarifa ni Izraiil, na mashahidi ni malaika wa mbinguni na ardhini, kisha mti wa Toba ukaambiwa utowe ulicho nacho, ukatoa duru nyeupe na yaquut nyekundu na zubrajad ya kijani na lulu.

Ulipo fika usiku baada ya ndoa, Mtume (s.a.w.w) akachukua farasi na akamuambia Fatuma: Panda, akamuamuru Salmaan amuongoze na mtume akawa anamuendesha, walipokua njiani Mtume (s.a.w.w) akasikia sauti, mara akamuona Jibrilu akiwa na malaika elfu sabini, na Mikaeli akiwa na malaika elfu sabini pia, Mtume (s.a.w.w) akawauliza, jambo gani limewaleta ardhini? Wakasema: tumekuja kumshingikiza Fatuma kwa Ali bun Abu Twalib, Jibrilu akasoma takbira na Mikaeli akasoma Takbira, na malaika wakasoma takbira na Mtume akasoma takbira, takbira zikasomwa kwa wingi katika usiku huo.

Hivyo ndio alivya taka Mwenyezi Mungu familia ya Mtume (s.a.w.w) iendelee kupitia Ali na Fatuma (a.s), matunda ya ndoa hiyo tukufu yakawa ni watoto watano, ambao ni Maimamu wawili watakasifu Hassan Almujtaba na Sayyid Shuhadaa Abu Abdillah Hussein (a.s), na mabinti wawili ambao ni Aqiilah bani Hashim Zainabu Alkubra na Ummu Kulthuum (a.s), walizaliwa katika uhai wa Mtume (s.a.w.w) ndani ya muda wa miaka tisa, na mototo wake wa mwisho ni Muhsin (a.s) aliyekufa kishahidi akiwa tumboni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: