asubuhi ya leo Jumamosi (1 Dhulhijja 1440h) sawa na (3 Agost 2019m) waziri wa ulinzi wa Iraq ametembelea makao mkuu ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, katika ziara hiyo ameona maendeleo ya kikosi katika upiganaji na upande wa teknolojia, kisha akatoa maoni yake kuhusu mustaqbali.
Mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Shekh Maitham Zaidi ameonyesha kufurahishwa kwao kutokana na ziara hii, akasema kua: “Tuna furaha kubwa kwa kutembelewa na Mheshimiwa waziri wa ulinzi Sayyid Najaah Shimri katika makao makuu ya kikosi cha Abbasi (a.s) ambapo tumemuonyesha hatua za kuanzishwa kwa kikosi hiki pamoja na mambo tuliyo fanya na tunayo tarajia kufanya”.
Akaongeza kua: “Tumemuonyesha kazi zinazo fanywa na kikosi katika kila sekta ikiwemo kifaru cha Alkafeel, tumemfafanulia uundwaji wake na teknolojia iliyo tumika pamoja na uwezo wa kifaru hicho, tumemuonyesha uwezo wote wa kikosi kwani, mafanikio yake ni sawa na wafanikio ya taifa la Iraq na sehi la serikali kwani kikosi hiki ni sawa na watumishi wa wanajeshi wa serikali”.
Fahamu kua kikosi cha Abbasi (a.s) Liwaau 26/Hashdi Sha’abi kilishiriki katika vita nyingi ya kukomboa ardhi ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, kilipewa majukumu mbalimbali ya kupigana na kikathibitisha uwezo wake katika uwanja wa vita, kutokana na mafundisho mazuri ya kijeshi waliyo nayo pamoja na siraha ya msimamo na Imani waliyo jufunza kutoka kwa kamanda wa jeshi la Imamu Hussein Abulfadhil Abbasi (a.s), katika vita hiyo kikosi kilitoa mashahidi wengi na majeruhi.