Maahadi ya Quráni tukufu imeanza kutekeleza mradi wa (Hafidhu Mahiri)

Maoni katika picha
Idara ya tahfiidh chini ya Maahadi ya Quráni tukufu ya Atabatu Abbasiyya asubuhi ya Jumapili (2 Dhulhijja 1440h) sawa na (4 Agost 2019m), imezindua masomo ya mradi wa (Hafidhu Mahiri) kwa wanafunzi wake, mradi huu unalenga kuimarisha uhifadhi wa Quráni tukufu.

Mradi huo upo ndani ya jengo la Alqamiy lililo chini ya Atabatu Abbasiyya, washiriki ni wale waliohifadhi juzuu kumi na kuendelea.

Washiriki wa mradi huu ni zaidi ya wanafunzi (25), unatarajiwa kufanyika kwa muda wa miezi miwili mfululizo, ndani ya muda huo wanafundishwa mambo muhimu yanayo wasaidia kua raia wema.

Fahamu kua uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeandaa kila kitu kinacho wezesha kufanyika kwa mradi huu, kuanzia walimu, kumbi za kusomea, sehemu za malazi ya wanafunzi, chakula na safari za kidini, kwa ajili ya kuhamasisha wanafunzi kushiriki katika mradi huu mtukufu.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu inafanya juhudi ya kusimamia mradi wa kuhifadhisha Quráni tukufu, hadi sasa inazaidi wa mahafidh (500) ndani na nje ya mkoa wa Karbala, inatumia mbinu za kisasa katika ufundishaji wake na inawalimu mahiri wenye uzowefu mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: