Idara ya mikakati na shughuli za utunzaji inafanya semina ya viongozi wa hazina ya Atabatu Askariyya tukufu…

Maoni katika picha
Idara ya mikakati na shughuli za utunzaji chini ya kitengo cha hazina (utunzaji) katika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya semina ya (kujenga uwezo kwa watumishi wa utunzaji) wa hazina za Atabatu Askariyya, semina hii ni sehemu ya kukamilisha mafunzo waliyopewa siku za nyuma.

Semina ilianza siku ya Jumapili (2 Dhulhijja 1440h) sawa na (4 Agoat 2019m) itaendelea hadi Alkhamisi wiki hii, katika semina hii wanafundishwa namna ya kutunza vifaa kale na umuhimu wake pamoja na majukumu ya kiongozi wa hazina ikiwa ni pamoja na kubaini kifaa kale na namna ya kukiingiza katika orodha ya vitu vilivyopo katika hazina ya makumbusho.

Fahamu kua kitengo cha hazina katika Atabatu Abbasiyya tukufu kila baada ya kipindi fulani huandaa semina za aina hii, pia huandaa vifaa kale na kuviingiza katika hazina ya makumbusho, kimekua kitengo muhimu kinacho kusanya kila kitu katika Ataba tukufu, kinatunza vifaa kale vya aina mbalimbali kwa kutumia mbinu za kisasa zinazo tumika na hazina za kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: