Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tawi la Najafu imefunga mradi wa semina za Quráni za majira ya kiangazi, katika hafla iliyo hudhuriwa na zaidi ya wanafunzi (4000) kutoka vitongoji mbalimbali, vikao vya kusoma Quráni vilifanyika katika vitongoji tofauti vya mkoa wa Najafu.
Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo fuatiwa na ujumbe kutoka kwa kiongozi wa tawi la Maahadi ya Quráni katika mji wa Najafu Sayyid Muhannad Almiyali, akaelezea ratiba ya mradi na masomo yanayo someshwa ambayo ni Quráni, Fiqhi na Akhlaq, akawashukuru watumishi wa tawi na maustadh wanao shiriki katika mradi kutokana na juhudu kubwa wanayo fanya.
Wanafunzi wa mradi wamefanya mambo mengi kwenye hafla hiyo, wamesoma Quráni tukufu kwa sauti nzuri, wameimba kaswada kuhusu kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na mwishoni mwa hafla wakapewa zawadi walimu wa semina pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri kisha wanafunzi wote wakapewa vyeti vya ushiriki wa semina.
Kumbuka kua mradi huu unalenga kutengeneza kizazi kinacho fuata muongozo wa vizito viwili Quráni tukufu na kizazi kitakatifu, na unashuhudia ongezeko la washiriki kila mwaka.