Kutokana na elimu za kisasa zinazo tegemewa: watalamu wa makumbusho ya Alkafeel wanaendelea kurepea siraha za kale

Maoni katika picha
Watalamu na watumishi wa makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na kazi ya kutengeneza (kurepea) siraha za kale zilizopo ndani ya makumbusho, zinazo onyeshwa na zisizo onyeshwa.

Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni makumbusho muhimu iliyo funguliwa katika Ataba mwaka (2009) wakati wa kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), inaidadi kubwa ya vifaa kale ambavyo historia yake inarudi miongo na miongo, jambo lililo sababisha watumishi wake wasomee mambo ya makumbusho ili waweze kutunza vizuri turathi zilizomo.

Miongoni mwa turathi zilizomo na zinazo fanyiwa matengenezo ni siraha za kale zinazo onyeshwa na zisizo onyeshwa, ambazo ni vielelezo vya vita zilizo piganywa zamani.

Kiongozi wa idara ya matengenezo Ustadh Aqiil Abbasi Hamdi ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu swala hili, amesema kua: “Hakika makumbusho ya Alkafeel inatoa umuhimu mkubwa sana kwa siraha za kale zilizopo ndani ya makumbusho kwa hiyo tumewaruhusu watumishi wetu kufanyia matengenezo siraha za kale zinazo hitaji matengeneza”.

Akaongeza kua: “Hakika matengenezo hayo yanafanywa kwa ustadi mkubwa, watumishi wanafanya kazi hiyo kwa umakini, kwa kiasi ambacho siraha haipotezi asili yake hata kidogo, kwani wanauzowefu mkubwa wa kufanya kazi za aina hii, wamehudhuria semina mara nyingi za kufundishwa namna ya kufanya kazi hio”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: