Mgahawa wa mkarimu unapanua huduma zake na unatumia vifaa vipya katika kuhudumia mazuwaru na umesisitiza kuwa lengo leke ni kutoa huduma bora kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhakikisha unatoa huduma bora kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), umeongeza huduma zake tukufu na umeongeza vifaa, kwa ajili ya kupokea idadi kubwa zaidi ya wageni wa malalo tukufu.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel umeongea na rais wa kitengo cha mgahawa (Mudhifu) bwana Aadil Hamaami ambaye ametuambia vitu vilivyo ongezwa hivi karibuni, amesema kua: “Mgahawa (Mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unaingia mamia ya mazuwaru kila siku, kuhudumia idadi kubwa ya watu kuna ugumu kidoga, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na kwa baraka za tunaye mtumikia pamoja na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tunaweza kupokea idadi kubwa ya mazuwaru, na vifaa hivi vitatusaidia kupokea idadi kubwa na kutoa huduma bora zaidi, itakayo waridhisha mazuwaru wanaokuja kubata baraka za chakula cha Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kua: “Miongoni mwa tuliyo ongeza katika siku za hivi karibuni ni:

  • - Mgahawa (Mudhifu) utakuwa wazi siku zote za wiki, hapo awali ulikua unafungwa siku moja kwa wiki hivi sasa haufungwi tena.
  • - Tumefungua madirisha ya ziada kwa ajili ya kugawa koponi za chakula ili kupunguza msongamano kwenye koponi, pamoja na kutengenisha sehemu za wageni na wairaq, wanaume na wanawake, sehemu hizo zimewekwa miamnvuli kwa ajili ya kuwastiri na jua pia kuna maji ya kunywa ya baridi.
  • - Tumeongeza muda wa kugawa koponi hadi saa sita mchana badala ya asubuhi tu, sasa zaairu anaweza kuchukua koponi na kwenda moja kwa moja katika ukumbi wa chakula au sehemu zinazo gawa chakula bila kuchelewa.
  • - Tunatoa maelekezo maalum kwa zaairu kuhusu sehemu na ukumbi anaotakiwa kwenda kupata chakula.
  • - Tumeongeza idadi ya watumishi ndani ya mgahawa na katika madirisha yanayo gawa chakula kwa nje.
  • - Tumefungua madirisha mapya ya kugawa chakula pindi ukumbi unapo jaa au kwa mazuwaru wanaopenda kubeba chakula.
  • - Tumeweka aina za vyakula vinavyo pendwa na mazuwaru wengi wa kiiraq na kigeni.
  • - Tuweka ukumbi maalum wa wanawake kwa ajili ya chakula, ambapo ukumbi wa ghorofani ni wa wanawake na ukumbi wa chini wa wanaume.
  • - Tumeandaa sehemu maalumu za wazee na watu wenye ulemavu zinazo endana na mazingira yao.
  • - Hivi sasa tunatengeneza program maalum ya kielektronik kwa aili ya kuoda chakula kimtandao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: