Katika program ya kujenga uwezo awamu ya tatu: Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel yatembelea malalo takatifu katika mji wa Najafu na yakutana na Maraajii watukufu

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka hema la Skaut katika mji wa Najafu kwa ajili ya wanachama wake wa kikosi cha Aljawwaalah kwenye program ya kuwajengea uwezo awamu ya tatu ambayo inawashiriki zaidi ya mia mbili (200).

Ratiba ya hema hilo imedumu kwa muda wa siku tatu na ilihusisha kutembelea malalo ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) pamoja na malalo ya Komail bun Ziyaad (r.a), ziara hizo zilihusisha swala za jamaa na mawaidha mafupi yaliyo kua yakitolewa baina ya swala mbili.

Kulikua pia na ratiba ya kutembelea Maraajii Dini wakuu katika mji wa Najafu, ambapo walipata nafasi ya kutembelea Maraajii wawili wakubwa ambao ni Sayyid Muhammad Saidi Hakiim na Aayatulluh Shekh Bashiri Najafiy, na wamepata fursa ya kusikiliza nasaha kutoka kwao moja kwa moja, kote walikua wanamaliza kwa dua ya kuiombea jumuiya ya Skaut ya Alkafeel iendelee katika mwenendo wa haki wa kumfuata Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: