Asubuhi ya mwezi (4 Dhulhijja 1440h) sawa na (6 Agost 2019m) katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar ametembelea malalo ya Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) akiwa na ugeni mzito, kisha wakaenda kumpongeza katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Hassan Shimri kwa kupewa cheo cha ukatibu mkuu wa Ataba hiyo.
Sayyid Ashiqar alimpa salamu maalum kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na watumishi wote wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kumuombea mafanikio mema katika kutumikia malalo ya Maiamamu wawili Aljawadaini (a.s) na kutoa kila aina ya huduma zinazo wezekana kwa mazuwaru watukufu.
Sayyid Ashiqar akamthibitishia kua; wahandisi, mafundi na watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya wapo tayali wakati wote kutoa aina yeyote ya msaada utakao ombwa kwao na Atabatu Kadhimiyya.
Fahamu kua watu walio fuatana na Sayyid Ashiqar katika ziara hiyo ni: mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Ustadh Jawaad Hassanawi, mshauri wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Twalaal Biir, rais wa kitengo cha mahusiano Ustadh Muiin Ahmadi Nasrullah, rais wa kitengo cha utumishi Ustadh Muhammad Aáraji pamoja na rais wa kitengo cha uangalizi wa haram Ustadh Nizaar Ghani.