Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wanaendelea na ujenzi wa maabara ya chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na kazi ya kujenga maabara ya chuo kikuu cha Al-Ameed, kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1600) ambapo wanajenga jengo la ghorofa nne, kiwango cha ujenzi hadi sasa ni zaidi ya asilimia thelathini (%30).

Tumeongea na kiongozi wa idara ya mambo ya nje katika kitengo hicho Mhandisi Hussein Alaa kuhusu mradi huu, amesema kua: “Kazi ya ujenzi wa Maabara ya chuo kikuu cha Al-Ameed inaendelea vizuri, ambapo tunajenga jengo la ghorofa nne kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1600)”.

Ujenzi huu unahusisha kumbi za maabara (14) na vyumba vya madarasa (12) pamoja na ukumbi wa mikutano wenye ukubwa wa mita za mraba (450) katika tabaka la chini, kuna sehemu mbili (2) za vyoo katika kila ghorofa, tabaka la chini linaurefu wa mita (6) huku matabaka mengine yakiwa na urefu wa mita tano (5).

Akaendelea kusema kua: “Tumemaliza hatua ya kwanza ambayo ilihusisha utowaji wa udongo wa juu pamoja na kusawazisha ardhi na kuweka sakafu ya zege, pia tumepiga ripu ukuta wa chini kwa smenti nyeupe na tumeweka tofali ndogo za sakafu”. Akasema: “Boma limejengwa kwa vyuma (Steel structures)”.

Kisha akasema: “Tayali tumeweka mfumo wa umeme na viyoyozi pamoja na mfumo wa mawasiliano na zimamoto, pia vifaa vyote vya maabara vimesha andaliwa, tunatarajia jengo hili litafunguliwa mwanzoni mwa mwaka ujao wa masomo”.

Fahamu kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo muhimu na kina idara nyingi, kinafanya kazi usiku na mchana kinahusika na matengenezo kwenye vitengo vyote vya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: