Pembezoni mwa hafla ya kuzindua dirisha la mazaru ya Qassim bum Kaadhim (a.s) kiwanda cha Saqaa chazindua vifaa vya kutengenezea dirisha la Maqaam ya Imamu wa zama (a.f)…

Maoni katika picha
Hafla ya kuzindua dirisha jipya la mazaru ya Qassim bun Imamu Mussa Alkaadhim (a.s), iliyo fanywa asubuhi ya Alkhamisi (6 Dhulhijja 1440h) sawa na (8 Agost 2019m) katika kiwanda cha Saqaa kinacho husika na kutengeneza madirisha na milango ya kwenye makaburi na mazaru tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, wamezindua vifaa vilivyo tengenezwa na kiwanda hicho kwa ajili ya kutengenezea dirisha lingine la Maqaamu ya Imamu wa zama (a.s).

Wasifu wa dirisha hilo ni:

  • 1- Linaupana wa (mita 6 na sm 6), na urefu wa (mita 3 na sm 25) takriban.
  • 2- Kiwango cha madini ya fedha kilicho tumika kinakaribia (kilo 88), na dhahabu ni zaidi ya kilo moja, inakaribia gram (1150).
  • 3- Yametumika madini mengine tofauti, ikiwemo (chuma) kopa na mbao bora kabisa.
  • 4- Aya iliyo andikwa inatoka katika surat Yunis.
  • 5- Limewekwa nakshi za mimea.

Fahamu kua mafundi wa kiwanda cha Saqaa kinacho husika na kutengeneza madirisha na milango ya makaburi na mazaru tukufu wataanza kutengeneza dirisha hilo mwishoni mwa mwezi huu wa Dhulhijja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: