Idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu yaviomba vyombo vya habari kutangaza msafara wa kutoa misaada katika mkoa wa Swalahu Dini

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetoa wito kwa watangazaji na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, kutangaza msafara wa kibinadamu utakaofanywa na kamati ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Swalahu Dini (Samaraa).

Taarifa iliyo tolewa kwa vyombo vya habari inasema kua:

Kwa watangazaji wote wa vyombo vya habari…

Tunaomba mtangaze msafara wa kibinadamu wa kwenda kusaidia ndugu zetu katika mkoa wa Swalahu Dini (Samaraa), ambao zitashiriki mawakibu za kusaidia kimkakati zilizopo katika mkoa huo zinazo fungamana na idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na msafara wa kibinadamu Alwafaa unaofanywa na Ataba tukufu, kwa maelekezo ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi chini ya usimamizi wa mkuu wa kikosi Shekh Maitham Zaidi.

Siku ya Ijumaa (9/ 8/ 2019m). ushiriki wenu utaonyesha mapenzi yenu kwa taifa na raia wake.

Kwa maelezo zaidi piga namba ifuatayo: (07707304392).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: