Ugeni kutoka idara ya maktaba tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea kitivo cha adabu katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya chini ya mradi wa kuhamasisha usomaji

Maoni katika picha
Ugeni kutoka idara ya maktaba tawi la wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umetembelea chuo kikuu cha Mustanswiriyya/ kitivo cha adabu, na kujadili mbinu zitakazo hamasisha wanafunzi wa chuo wapende kusoma vitabu, pamoja na kuinua kiwango cha uzalendo na kujivunia utaifa wao, kupitia harakati ya kuhamasisha usomaji wa vitabu.

Kiongozi wa idara ya maktaba tawi la wanawake bibi Asma Raádi Al-abadi amesema kua: “Ziara hii ni sehemu ya harakati za idara chini ya ofisi ya kushawishi usomaji wa vitabu, tumechagua baadhi ya vyuo vikuu kwa baadhi ya wanafunzi na wao ndio njia ya kuifikia jamii katika kila sekta, tunatarajia ziara hii kua chachu ya kuendelea kushirikiana zaidi”.

Naye mkuu wa kitivo cha adabu Dokta Farida Jaasim amesema kua: “Kupitia ratiba ya kuhamasisha usomaji tutapata faida nyingi, ikiwa ni pamoja na kua na wanafunzi wa chuo wanao jitambua wawapo ndani au nje ya chuo, jambo la pili ugeni huu kutoka katika idara ya maktaba tawi la wanawake katika Ataba tukufu ni mafanikio makubwa kwa chuo”.

Akaongeza kua: “Hakika ugeni huu ni heshima kubwa kwa chuo hiki kutokana na mambo muhimu waliyo nayo kuhusu jamii hasa tabaka la vijana”.

Akasema: Uongozi wa kitivo cha adabu upo tayali kupanua wigo wa mradi wa kuhamasisha usomaji unao saidia kutengeneza kizazi chenye elimu na maadili mazuli katika sekta tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: