Mawakibu za watu wa Karbala zinaomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa Karbala wamezowea kuomboleza vifo vya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kwa mawakibu za matam na zanjiil kama sehemu ya kufanyia kazi maneno ya Imamu Swadiq (a.s) yasemayo: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu).

Asubuhi ya Ijumaa (7 Dhulhijja 1440h) sawa na (9 Agost 2019m) zimejitokeza mawakibu za matam na zanjiil katika mji wa Karbala kumboleza kifo cha Imamu wa tano Muhammad bun Ali Albaaqir (a.s) kutoka sehem tofauti za mji huo, wakiwa wamebeba jeneza la kuigiza kama la Imamu madhlumu aliye uwawa kwa sumu, wakaelekea kwenye kaburi la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwenda kuwapa pole pamoja na kumpa pole Imamu wa zama (a.f) kwa msiba huu.

Huku wakiwa wamejaa huzuni na majonzi makubwa wametembea hadi kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kabla ya kwenda katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), wameanza kupita katika malalo ya mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s) na kiongozi wa jeshi lake na alikua ndio mlango wa kuelekea kwa Imamu Hussein (a.s), wameingia ndani ya haram yake tukufu na kumpa pole, halafu wakaelekea katika malalo ya baba wa watu huru (a.s) kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakiimba kaswida za huzuni na kupiga vifua vyao, hadi walipofika katika malalo ya Abu Abdillahi (a.s) na kufanya majlis ya kuomboleza.

Fahamu kua watu wa mji wa Karbala wamezowea kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa kufanya matembezi ya kuomboleza au kutoa huduma ya chakula na vinywaji kwa mazuwaru katika siku za maombolezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: