Kufanyika kwa majlis za kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) viongozi na marais wa vitengo pamoja na watumishi wa kawaida, leo asubuhi (7 Dhulhijja 1440h) sawa na (9 Agost 2019m) wamefanya majlis ya kuomboleza kifo cha Imamu wa tano Muhammad Albaaqir (a.s).

Majlis hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala na kuhudhuriwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo fuatiwa na mawaidha kutoka kwa Mheshimiwa Shekh Muhsin Khaqaani mtumishi wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, akazungumzia kifo cha Baaqir Uluum (a.s).

Hali kadhalika ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ilifanywa majlis nyingine iliyo endeshwa na masayyid wanaofanya kazi katika Ataba tukufu na kuhudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru waliokuja kumpa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na kufuatiwa na mawaida yaliyo tolewa na Sayyid Mudhwar Qazwini.

Fahamu kua Imamu Baaqir (a.s) alizaliwa katika mwezi wa Rajabu mwaka (57) hijiriyya huko Madina, na akafariki mwezi (7) Dhulhijja mwaka wa (114) hijiriyya kwa sumu, na akazikwa katika makaburi ya Baqii Gharqad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: